Simba imemtambulisha beki wa kushoto, Nickson Kibabage ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili.
Ikumbukwe siku chache zilizopita uongozi wa Singida Black Stars alikokuwa akikipiga nyota huyo ulitoa taarifa kwa umma kama wamewapa bure Simba mkali huyo.
Upande huo wa kushoto anaungana na Anthony Mligo.
Kibabage amewahi kuhudumu katika timu mbalimbali zikiwemo Mtibwa, Diffaa El Jadid ya Morroco, KMC na Mabingwa wa Ligi kuu Tanzania bara Yanga.
#StarTvUpdate