Zaidi ya watu 39 wamefariki na wengine kujeruhiwa siku ya Jumapili, Januari 18, kusini mwa Uhispania, kulingana na ripoti mpya ya vifo iliyothibitishwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Uhispania, wakati treni moja ilipoacha njia yake na kugongana na treni nyingine. Huduma ya usafiri wa treni za mwendo kasi zimesitishwa angalau hadi Jumatatu, Januari 19, kati ya Madrid na miji kusini mwa nchi. Rais Pedro Sánchez amezuru eneo la tukio.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Treni mbili za mwendo kasi ziliacha njia Jumapili, Januari 18, kusini mwa Uhispania na kugongana, imesema kampuni inayosimamia huduma za usafiri wa treni za mwendo kazi, Adif. Angalau watu 39 wamefariki katika ajali hiyo, kulingana na ripoti mpya ya vifo iliyotolewa na Guardia Civil, na kufanya kuwa ajali mbaya zaidi ya treni kuwahi kutokea nchini Uhispania tangu mwaka 2013. Ajali hiyo pia ilisababisha watu 122 kujeruhiwa, 48 kati yao wanaendelea kulazwa hospitalini na 12 wakiwa katika uangalizi maalum, kulingana na idara ya huduma za dharura.

Abiria wapatao 300 walikuwa ndani ya treni hizo, kulingana na wenzetu huko El Pais. Mamlaka za kikanda za Andalusia zinaripoti angalau watu 73 wamejeruhiwa. Waziri wa Uchukuzi wa Uhispania Oscar Puente ameonya kwenye mitandao ya kijamii kwamba “ajali ilikuwa mbaya” na kwamba idadi ya vifo inaweza kuongezeka kutokana na “taarifa za kutisha sana” kuhusu ajali hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *