Wananchi jijini Mwanza wamesema Daraja la Mkuyuni lililopo Wilaya ya Nyamagana litakapofunguliwa rasmi kwa matumizi litakuwa msaada mkubwa kwao, hususan wakati wa kipindi cha mvua, kwani litarahisisha usafiri na usafirishaji wa huduma muhimu.
Daraja hilo lililojengwa na mkandarasi Jasco Co. Ltd limekamilika na tayari limekabidhiwa kwa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kwa ajili ya uangalizi na taratibu nyingine za kuanza kutumika.
#AzamTVUpdates
✍Innocent Aloyce
Mhariri | John Mbalamwezi