‎Yanga imeendeleza wimbi la ushindi Ligi Kuu NBC Tanzania Bara wakati huu kichapo kikienda kwa wajeda,Mashujaa FC.

‎Sio tu Yanga imeshinda na kuondoka na alama tatu bali imetoa na burudani ya mpira, matokeo makubwa.

‎Kivutio zaidi kwa Wananchi ni straika wao mpya, Maria Depu kutoka Ligi Kuu Poland kufanikiwa kufunga mechi yake ya kwnza, lakini pia akitoa assist.

‎Kiufundi Yanga pamoja na ushindi mkubwa ambao wameuvuna bado wamecheza mpira wa kitabuni bila kupoteza nishati kubwa sana.

‎Imecheza objective football. Haijataka kukimbazana sana uwanjani wala kugongana sana, wala kuwa na matamanio kumiliki mali nga nga nga, walistiki kwenye vitu muhimu.

‎Kwa upande wa Mashujaa ilikuwa na makosa mengi ya kiulinzi hasa kukaba kwa macho, huku ikipoteza mipira mara kadhaa kirahisi wakati wa maandalizi ya shambulizi kutokea katikati ya Uwanja.

‎Full Time

‎Yanga 6-0 Mashujaa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *