Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi Komredi Kenan Kihongosi, ameendelea kusikiliza na kuzitafutia ufumbuzi kero mbalimbali za wananchi ambazo amekua akizipokea katika mikutano yake kwenye ziara anayoendelea nayo mkoani Singida.Pia ametaka Watumishi wazembe wachukuliwe hatua.

Mwenezi Kihongosi amesema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika Stendi ya zamani mkoani Singida.Akizungumza na wananchi, amewataka watumishi kupitia changamoto anazozipokea katika mikutano yake, wajipime juu ya utendaji wao wa kazi.Pia Komredi Kihongosi amewataka wasifanye kazi kwa mazoea kwani CCM haitafumbia macho uzembe wa aina yoyote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *