Katika kukuza uwekezaji visiwani Zanzibar, Rais Dkt. Hussein Mwinyi amesema serikali yake imejipanga kuhakikisha inaweka mazingira bora ya uwekezaji, kuweka vivutio vya kodi na kuondoa urasimu.

Rais Mwinyi ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa boti mpya ya kisasa ya Kilimanjaro IX – The Dragon of the Sea, yenye uwezo wa kubeba abiria 631 kwa wakati mmoja.

Uzinduzi huo umefanyika katika fukwe zilizopo viunga vya Hotel Verde, mkoa wa Mjini Magharibi, na umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, wadau wa sekta ya usafirishaji pamoja na wananchi.

#AzamTVUpdates
✍Jairo Mtitu
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *