Muasisi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mzee Edwin Mtei amefariki dunia.
Mzee Mteai ambaye pia alikuwa Gavana wa kwanza wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), amefariki usiku wa kuamkia leo Jumanne, Januari 20,2026 akiwa na umri wa miaka 94 baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Taarifa kutoka ndani ya chama hicho zinasema kuwa Mzee Mtei amefariki akiwa njiani katka gari ya wagonjwa akipelekwa katika Hospitali ya Seliani baada ya kuzidiwa.
Taarifa ya Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Bara, John Heche imesema kuwa chama hicho kimepoteza moja ya nguzo yake imara.
Mzee Mtei alichaguliwa kuwa Gavana wa kwanza Tanzania mwaka 1966 na miaka 12 baadaye aliteuliwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango.
#StarTvUpdate