DAR ES SALAAM; NAIBU Meya wa Manispaa ya Kigamboni, Elizabeth Kimambo amefurahishwa na wadau walioandaa mapambano ya ngumi na kusema kuwa wataiheshimisha manispaa hiyo.

Kimambo alisema hayo alipokuwa mgeni rasmi mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa M Garden kulipofanyika mapambano ya mchezo huo.

“Mapambano haya yataitangaza wilaya yetu na pia kuiheshimisha katika medani ya mchezo wa ngumi hapa nchini, hivyo niwapongeze waandaaji wa tukio hili,”alisema.

Aliongeza kuwa waandaaji hao wamapaswa kufanya mashindano hayo mara kwa mara, ili kukuza zaidi vipaji vya mabondia wa Kigamboni na milango ipo wazi kwa ajili ya kuwezesha kufanikisha hilo.

Naye Diwani wa Kata ya Mjimwema, Omary Ngulangwa akizungumza katika tukio hilo alisema serikali iko bega kwa bega na wadau wa michezo katika kukuza vipaji vya michezo yote.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Braso Sports Promotion iliyoandaa tukio hilo, Kivuri Chuma ‘Shadow” alisema kampuni yake imedhamiria kuwafikisha mbali mabondia kutoka Kigamboni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *