Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hissein Ali Mwinyi amezindua rasmi boti ya kisasa ya abiria ijulikanayo kama Kilimanjaro IX – The Dragon of the Sea, yenye uwezo wa kubeba abiria 631 kwa wakati mmoja.

Uzinduzi wa boti hiyo ni hatua muhimu katika kuimarisha sekta ya usafiri wa majini na kuboresha huduma kwa wasafiri kati ya Zanzibar na maeneo mengine.

Uzinduzi huo umefanyika katika fukwe zilizopo katika viunga vya Hotel Verde, iliyopo mkoa wa Mjini Magharibi, na umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, wadau wa sekta ya usafirishaji pamoja na wananchi.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *