DAR ES SALAAM: MSEMAJI wa Klabu ya Simba SC, Ahmed Ally, amewaomba mashabiki wa klabu hiyo kumpokea na kumpa ushirikiano beki wa kushoto Nikson Kibabage, akisisitiza kuwa ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa wa kuisaidia timu.
Katika taarifa yake aliyoitoa leo Januari 20,2026, Ahmed amesema Kibabage ana ubora na uwezo ambao endapo atapewa sapoti inayostahili, ataifanyia makubwa Simba.
“Tumpokee kijana wetu, tumpe ushirikiano. Kwa uwezo na ubora alikuwa nao, atatufanyia makubwa sana ndani ya timu yetu,” alisema Ahmed.
Nikson Kibabage alitambulishwa rasmi jana kama mchezaji mpya wa Simba, baada ya kusajiliwa katika dirisha hili la usajili akitokea Singida Black Stars.
