
Kwa mara nyingine tena, mashirika ya kiraia ya Kenya yamekuwa sauti ya wenzao wa Uganda. Mnamo Januari 19, 2026, walifanya mkutano na waandishi wa habari jijini Nairobi kukemea vurugu zilizokumba uchaguzi mkuu wa Januari 15. Mnamo Januari 17, Yoweri Museveni alishinda muhula wa saba wa urais kwa zaidi ya asilimia 71 ya kura.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu jijini Nairobi, Gaƫlle Laleix
Licha ya kutangazwa kwa matokeo, hali ya hofu bado inatawala nchini Uganda, kulingana na Mwanase Ahmed wa shirika la Afrika Mashariki Jumuiya Ni Yetu: “Tunajua kwamba watu 100 walifikishwa mbele ya mahakama jijini Kampala jana. Wengine wanazuiliwa. Viongozi kadhaa wa Jukwaa la Umoja wa Kitaifa wametekwa nyara na bado hawajulikani walipo.” Leo, takriban watu 1,000 wamekamatwa na hawajulikani walipo.
Mashirika ya kiraia ya kikanda pia yanaripoti vifo 60 tangu uchaguzi huo. Ukandamizaji huu ulitekelezwa kwa sehemu kubwa na “vikosi vya ghetto,” wanamgambo wanaotumikia utawala, kulingana na mtetezi wa haki za binadamu Cyprian Nyamwamu: “Waliwapa silahai, wakawafunza, na kuwapa uhuru wa kuwatisha na kuwanyanyasa watu siku ya uchaguzi. Wao ndio waliowakamata maafisa katika vituo vya uchaguzi na kuwafanya watoweke. Na mtoto wa Museveni hafichi. Yote yako kwenye mitandao yake ya kijamii.”
“Umoja wa Afrika huchagua kuishi kwa madikteta”
Mashirika ya kiraia yanalaani ukimya wa taasisi za Kiafrika na kikanda kuhusu vurugu hizi. Cornelius Oduor wa Tume ya Haki za Binadamu ya Kenya ameshtumu: “Kwa kukubali matokeo ya 71.6%, huku mitandao ya Uganda ikizimwa na familia ya kiongozi wa upinzani Bobi Wine ikibaki kizuizini, na kwa kumpongeza Yoweri Museveni, Umoja wa Afrika unachagua kuishi kwa madikteta badala ya maisha ya raia wa Afrika.”
Mnamo Januari 19, marais wa Somalia, Rwanda, na Kenya walimpongeza Yoweri Museveni kwa kuchaguliwa kwake tena.
Mbabe huyo wa zamani wa vita vya msituni, Yoweri Museveni, mwenye umri wa miaka 81 alishinda muhula wa saba mfululizo kwa kupata asilimia 71.65 ya kura, kulingana na matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa rais yaliyotolewa Jumamosi na tume ya uchaguzi. Bobi Wine, aliyepata asilimia 24.72 ya kura na ambaye alielezea ” kufutilia mbali kabisa matokeo yaliyoibiwa”, alibaini kwamba aliamua kujificha baada ya uvamizi wa vikosi vya usalama nyumbani kwake.