Afrika Kusini imetuma timu kusaidia juhudi za uokoaji baada ya mwanasiasa wa eneo hilo kusombwa na mafuriko alipokuwa akizuru nchi jirani ya Msumbiji.

Andile Mngwevu, diwani katika manispaa ya Ekurhuleni, mashariki mwa Johannesburg, na wengine wanne walikuwa katika jimbo la Gaza nchini Msumbiji wakati gari lao lilipokumbwa na mafuriko, maafisa wanasema.

Ni mmoja tu wa abiria ambaye amegunduliwa “hadhi na mahali walipo abiria wengine bado haijathibitishwa”, manispaa ilisema katika taarifa.

Mafuriko yameharibu sehemu za nchi zote mbili na kusababisha Rais wa Msumbiji Daniel Chapo kufuta safari yake ya Mkutano wa Kiuchumi wa Dunia huko Davos.

Msumbiji imetangaza tahadhari ya hali ya ta dharura kutokana na mafuriko makubwa huku Afrika Kusini ikitangaza janga la kitaifa.

Msimu wa mvua umeanza katikati na kaskazini mwa Msumbiji, na utabiri wa mvua kubwa zaidi katika sehemu kubwa za nchi, ambayo inaingia msimu wake wa kila mwaka wa vimbunga.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *