Naibu waziri wa viwanda na biashara Dennis Londo amerirdhishwa na hatua za ufufuaji wa kiwanda cha kutengeneza vipuli na mashine kwaajili ya viwanda cha Kilimanjaro Machine tols na kuahidi kuwa,Serikali itaendelea kukiwezesha kiwanda hicho kilichopo wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro ili kuokoa fedha ambazo serikali ingezitumika kuagiza vifaa hivyo nje ya nchi kwa gjharama kubwa.

Amebainisha hayo alipotembelea kiwanda hicho ambapo amesema serikali imewekeza fedha ili kiwanda hicho,kuzalishe malighafi kwaajili ya viwanda nakwamba kitainua uchumi wa nchi na kuwapatia Watanzania ajira huku akiutaka uongozi kufikisha maeneo ya vijijinj mashine na mitambo inayotengenezwa.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *