Ugonjwa wa ukoma huanza taratibu na dalili zake mara nyingi huonekana baada ya muda mrefu, hali inayofanya baadhi ya wagonjwa kuchelewa kugundulika.

Dalili za awali hujumuisha kuonekana kwa mabaka kwenye ngozi yenye rangi tofauti na ngozi ya kawaida, ambayo mara nyingi haina hisia za maumivu au joto. Ngozi inaweza pia kuwa kavu, kukaza au kupoteza uwezo wa kutoa jasho katika maeneo yaliyoathirika.

Kadri ugonjwa unavyoendelea, mgonjwa anaweza kupata ganzi kwenye mikono, miguu au sehemu nyingine za mwili kutokana na kuathirika kwa mishipa ya fahamu. Kufahamu zaidi, ungana na Mtaalamu wa ugonjwa wa ukoma, Dkt. Deus Kamala.

#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *