Umoja wa Ulaya (EU) umetoa euro milioni 2  kama msaada kusaidia jamii zilizoathiriwa na mgogoro katika mkoa wa Kivu Kusini, Mashariki mwa DRC kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa Jumatano, Januari 21. Ufadhili huo utatoa msaada muhimu kwa maelfu ya watu wanaohitaji msaada wa dharura, hati hiyo inasema.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mgogoro unaochochewa na vita kati ya jeshi la DRC, FARDC na washirika wake na waasi wa AFC/M23 unaoendelea nchini DRC, haswa katika maeneo ya Uvira, Fizi, na Kalehe, umesababisha takriban watu 500,000 kyahaa makazi yao, wakiwemo zaidi ya 90,000 ambao wamekimbilia nchi jirani ya Burundi, idadi ambayo inaendelea kuongezeka kila siku, EU inabainisha kulingana na Radio Okapi.

Kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari, mradi huu wa kukabiliana na dharura utatekelezwa hadi mwisho wa mwezi Juni 2026 na utawanufaisha watu waliohamishwa ndani ya nchi katika maeneo yaliyoathiriwa zaidi ya Uvira, Fizi, na Kalehe. Ufadhili wa EU utaunga mkono juhudi za washirika wake, wakiongozwa na muungano wa SAFER (Acted, Concern Worldwide, Mercy Corps, Baraza la Wakimbizi la Norway, na Solidarités International), kutoa msaada muhimu, kwa kuzingatia usaidizi wa pesa taslimu, ulinzi, maji, usafi wa mazingira, na hatua za usafi.

Mgogoro mashariki mwa DRC unaendelea kusababisha watu wengi kutoroka makazi yao katika mkoa wa Kivu Kusini na kukimbilia nchi jirani, huku maelfu wakikimbia ghasia zinazoendelea na rasilimali za ndani zikipungua, EU imehitimisha katika taarifa yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *