Marekani inaendesha operesheni za kuhamisha hadi wafungwa 7,000 kutoka kundi la Islamic State (ISIS) nchini Syria kwenda nchi jirani ya Iraq ili “kuhakikisha kwamba magaidi wanabaki katika magereza salama,” jeshi la Marekani limetangaza siku ya Jumatano.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Vikosi vya Marekani vilifanikiwa kusafirisha wapiganaji 150 wa ISIS wanaozuiliwa katika gereza huko Hassakeh, Syria, hadi eneo salama nchini Iraq. Kwa jumla, hadi wafungwa 7,000 wa ISIS wanaweza kuhamishwa kutoka Syria kwenda vituo vinavyodhibitiwa na Iraq,” Kamandi Kuu ya Marekani (CENTCOM) imeandika katika taarifa iliyochapishwa kwenye jmtandao wa kijamii X.

Mkuu wa vikosi vya Marekani Mashariki ya Kati Brad Cooper katika taarifa amesema kuwa amezungumza na Rais wa Syria Ahmed al-Sharaa ili kuhakikisha kwamba wanajeshi wa Syria na vikosi vyengine haviutatizi mchakato huo.

Kuna zaidi ya wafungwa 10,000 wanachama wa IS na maelfu ya wanawake na watoto walio na mafungamano na kundi hilo la kigaidi katika magereza ya Syria.

Siku ya Jumanne, Syria ilitangaza usitishwaji wa mapigano na vikosi vya Wakurdi na kuwapatia siku nne kukubali kujiunga na serikali kuu, jambo ambalo Marekani iliwataka walikubali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *