Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo amevunja mgomo wa wafanyakazi zaidi ya 1,500 wa kiwanda cha NAMERA kilichopo Gongolamboto Dar es Salaam, baada ya wafanyakazi hao kulalamikia mishahara midogo isiyoendana na tamko la Serikali la kima cha chini cha mshahara.
Akizungumza na wafanyakazi na uongozi wa kiwanda hicho, DC Mpogolo amesema mishahara italipwa kwa mujibu wa mpango wa Serikali, akisisitiza kuwa haki za wafanyakazi zitalindwa na kuwataka viongozi wa kiwanda kuwa na mahusiano mazuri na wafanyakazi wao.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi
(Feed generated with FetchRSS)