
Nchini Msumbiji, hali ya kibinadamu inaendelea kuzorota kutokana na mafuriko ambayo yamekuwa yakiikumba nchi hiyo kwa wiki kadhaa. Idadi ya vifo imeongezeka tena: mamlaka sasa inaripoti vifo 114. Taasisi ya Kitaifa ya Hali ya Hewa ya Msumbiji (INAM) ilitoa tahadhari nyingine siku ya Jumanne, Januari 21.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu jijini Nairobi, Gaƫlle Laleix
Kulingana na jarida la hivi punde la INAM lililochapishwa siku ya Jumanne, mdororo wa kitropiki unatarajiwa kugonga kusini mwa nchi tena katika saa zijazo. Mvua kubwa ikiambatana na upepo mkali inatabiriwa.
Msumbiji imeingia katika msimu wa kimbunga, na mvua zilizokusayika tangu mwezi Oktoba zimesababisha mafuriko makubwa, na kutumbukiza maeneo mengi katika hali mbaya ya kibinadamu.
Kulingana na ripoti ya hivi karibuni kutoka Taasisi ya Kitaifa ya Usimamizi na Kupunguza Hatari za Maafa, karibu watu 700,000 wameathiriwa na mafuriko kote nchini.
Zaidi ya nyumba 11,000 zimeharibiwa kwa kiasi, huku takriban nyumba 5,000 zikiwa zimebomolewa kabisa.
Vituo vya mapokezi vimeanzishwa ili kuwahifadhi walioathiriwa. Kwa sasa vinahifadhi karibu watu 89,000, “nusu yao ni watoto,” anaelezea Guy Taylor, afisa wa mawasiliano wa UNICEF nchini Msumbiji.
Masuala ya afya na chakula
Shirika la Umoja wa Mataifa lina wasiwasi kuhusu hatari ya kuenea kwa magonjwa, yanayosababishwa na maji yaliyotuama, pamoja na mgogoro mkubwa wa chakula. Maeneo makubwa ya kilimo kwa sasa yamejaa maji.
“Magonjwa yanayosababishwa na maji na utapiamlo huunda mchanganyiko hatari,” anaonya Guy Taylor. Anasema kwamba hata kabla ya mafuriko, watoto wanne kati ya kumi wa Msumbiji walikuwa tayari wana njaa.