Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta Samia Suluhu Hassan, ataongoza zoezi maalum la upandaji miti litakalofanyika Januari 27 mwaka huu, maeneo ya Bungi Kilimo na Kizimkazi, Zanzibar, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa.
Zoezi hilo lenye kauli mbiu “Uzalendo ni Kutunza Mazingira, Shiriki Kupanda Miti” linaakisi dhamira ya Rais Dokta Samia katika kuendeleza ajenda ya Taifa ya uhifadhi na utunzaji wa mazingira.
Ikiwemo upandaji miti, ulinzi wa vyanzo vya maji, kuimarisha uoto wa asili, na kuchangia kwa vitendo juhudi za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Zoezi hilo ni ishara ya uwajibikaji wa pamoja na linatoa fursa kwa kila mmoja, kwa nafasi yake na mahali alipo, kushiriki katika kulinda na kuenzi mazingira kwa manufaa ya sasa na kizazi kijacho.
Aidha, Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, inawahimiza wananchi, taasisi na wadau wa mazingira kuunga mkono dhamira ya Rais kwa kuendeleza ajenda ya uhifadhi wa mazingira, ikiwemo kupanda angalau mti mmoja nyumbani, shuleni, kazini, au kwenye maeneo ya jamii.

(Feed generated with FetchRSS)