Serikali imezihimiza taasisi za fedha kubuni, kutoa bidhaa na huduma zitakazowagusa wananchi moja kwa moja na kutoa elimu ya kifedha kwa wananchi ili kuongeza uelewa na matumizi sahihi ya huduma za benki, ili kukuza uchumi jumuishi na shindani.

Akizungumza katika viwanja vya Usagara, mkoani Tanga kunakofanyika maadhimisho ya wiki ya huduma za fedha kitaifa, Naibu Waziri wa Fedha, Laurent Luswetula, ameipongeza Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) na taasisi nyingine za kifedha kwa mchango wao katika kuimarisha sekta ya fedha.

Amesema kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa taasisi hizo na kuwahimiza wananchi kutumia fursa za huduma za kifedha zinazotolewa nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi, amesema benki hiyo imejikita katika kubuni huduma jumuishi na bunifu za kifedha. Huduma hizi zinawalenga wafanyabiashara, wajasiriamali, wakulima, wawekezaji na taasisi mbalimbali ili kuongeza ushiriki wa wananchi katika shughuli za uzalishaji na maendeleo ya Taifa.

Sabi ameongeza kuwa NBC inaendelea kutoa mikopo kwa sekta za kipaumbele ikiwemo kilimo, biashara, viwanda na miradi mikubwa ya kimkakati. Benki hiyo pia imewekeza katika teknolojia za kisasa za kifedha (FinTech) ili kuongeza upatikanaji wa huduma, hususan kwa wananchi waishio vijijini.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *