Wiki moja baada ya uchaguzi nchini Uganda, kesi ya Sarah Bireete imesitishwa. Mahakama imeahirisha uamuzi wake kuhusu dhamana ya wakili huyu mwenye ushawishi na mwanaharakati wa haki za binadamu hadi Januari 28, ikisema inataka kuchunguza hoja zilizotolewa na upande wa utetezi na upande wa mashtaka.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Sarah Bireete ambaye alikamatwa Desemba 30 mjini Kampala, mji mkuu wa Uganda, kuelekea uchaguzi wa urais na wa wabunge, alifika mbele ya mahakama ya Buganda Road siku ya Jumatano, Januari 21. Anashtakiwa kwa “madai ya kufichua data ya wapiga kura bila idhini kutoka kwa Tume ya Uchaguzi”—shutuma anayokana. Wafuasi wake wanalaani kuendelea kwake kuzuiliwa.

Mahakamani, upande wa utetezi na upande wa mashtaka walikabiliana poiti kwa pointi. Upande wa mashtaka unakataa, haswa, sababu za kimatibabu zilizotolewa na upande wa utetezi: Sarah Bireete anadai kuwa na shinikizo la damu, lakini, kulingana na upande wa mashtaka, “hakuna ushahidi kwamba Mamlaka ya gereza haiwezi kumtibu.” Upande wa mashtaka pia unataja “hatari ya vitisho vya mashahidi na kuhoji uwezo wa kifedha wa wadhamini.”

Uchapishaji wa taarifa za wapiga kura unaoshukiwa

Mbali ya vita hivi vya kisheria, upande wa mashtaka wenyewe unamtuhumu mwandishi wa habari na mwanaharakati Agather Atuhaire: kiini cha jambo hilo ni uchapishaji unaodaiwa wa taarifa za wapiga kura—bila idhini ya Tume ya Uchaguzi.

“Kwa kweli, huu ni uhalifu gani? Alichukua taarifa hizi kutoka kwa tovuti ya Tume ya Uchaguzi na kuzishiriki na umma. Zilitakiwa kupatikana kwenye tovuti hiyo,” anasema. Ikiwa kuna sababu ambazo hawakutaka Sarah Bireete aachiliwe huru, ni kwamba sababu hii haijaisha—na wengi walidhani ilikuwa inahusiana na uchaguzi. Nilitumaini wangemwachilia leo. Lakini kwa kuwa ukandamizaji baada ya uchaguzi, kwa maoni yangu, ni mbaya zaidi kuliko hapo awali, nadhani wanataka kuendelea kuwazuia wale wote wanaokosoa kinachoendelea hivi sasa.

“Kamatakama inaongezeka” Agather Atuhaire anaelezea kinachoendelea hivi sasa kama ugumu wa hali tangu uchaguzi: kulingana na yeye, “kamatakama inaongezeka, haswa miongoni mwa wafuasi wa upinzani, na vurugu zimeripotiwa katika vitongoji kadhaa.” Kuhusu utaratibu huo, mwanaharakati huyo anasema kwamba Sarah Bireete mwanzoni aliwekwa kizuizini kwa siku kadhaa bila mashtaka kabla ya hatimaye kushtakiwa, na kwamba mahakama tayari iliipa ofisi ya mwendesha mashtaka wiki kadhaa kujibu ombi la dhamana.

Hatimaye, Agather Atuhaire anaonyesha kufanana kati ya kesi ya Sarah Bireete na ile ya kiongozi wa upinzani Kizza Besigye, na wafuasi wa chama cha NUP cha kiongozi wa upinzani Bobi Wine – ambao, anasema, “wamekamatwa kwa miaka mingi bila kushtakiwa.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *