Victor Mhagama, mtoto wa aliyekuwa mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama ameibuka mshindi katika kinyang’anyiro cha kura za maoni kuwania ubunge katika jimbo hilo.
Kijana huyo ameibuka mshindi katika mchakato wa kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kufuatia kifo cha mama yake Jenista aliyefariki hivi karibuni na jimbo hilo kuwa wazi.
Victor alitangazwa mshindi katika uchaguzi uliomalizika jana saa 5 usiku na kuwashinda makada wengine 26 waliojitokeza kuwania nafasi hiyo.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa CCM Wilaya ya Songea Vijijini,
Juma Nambaila amemtangaza Victor
kuwa mshindi kwa kupata kura 3,040 kati ya 8,577zilizopigwa kwenye kata 16 za jimbo hilo.
#StarTvUpdate

(Feed generated with FetchRSS)