Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), siku sita baada ya kukamatwa kwake, sasa kuna habari kuhusu Aubin Minaku. Kulingana na washirika wake, makamu wa rais wa chama cha PPRD cha Joseph Kabila na naibu spika wa zamani wa Bunge la taifa kwa sasa anashikiliwa na Baraza la kitaifa la ulinzi wa mtandaoni, kitengo cha idara ya ujasusi kilio chini ya amri ya rais wa jamhuri. 

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Aubin Minaku inaripotiwa anashikiliwa katika jumba linalodhibitiwa na Baraza la kitaifa la ulinzi wa tandaoni, kulingana na washirika wake. Mkewe aliweza kumuona kwa mara ya kwanza siku ya Jumanne, Januari 20, kulingana na vyanzo vyetu. Hata hivyo, katika hatua hii, sababu sahihi za kukamatwa kwake bado hazijawasilishwa kwake, kulingana na duru kadhaa zinazoaminika.

Hata hivyo, mawakili wake bado hawana uwezo wa kumfikia. Kukamatwa huku ni sehemu ya mfululizo wa kamatakamata inayowalenga viongozi wa chama cha Joseph Kabila na washirika wake kadhaa wa tangu mwezi uliopita.

Ndani ya PPRD, baadhi ya vyanzo pia vinabaini kwamba kukamatwa huku kunaweza kuhusishwa na uhamasishaji mnamo Januari 16, kumbukumbu ya kuuawa kwa Laurent-Désiré Kabila, baba yake Joseph Kabila.

Hali ni tofauti kwa Emmanuel Ramazani Shadary. Yeye pia alikamatwa na kuwekwa kizuizini na idara hiyo, kulingana na familia yake. Amenyimwa uhuru wake kwa zaidi ya mwezi mmoja tu. Licha ya juhudi za kuwasiliana naye, wala mkewe wala mawakili wake hawajaruhusiwa kumuona. Mkewe anadai kuwa ameandika barua kwa Baraza la kitaifa la ulinzi wa mtandaoni, lakini hajapata jibu hadi sasa. Hata hivyo, anaendelea kumletea mumewe chakula kila siku katika makao makuu ya CNC.

Wanachama wengine wawili wa PPRD pia wanashikiliwa tangu mwezi Desemba: Dunia Kilanga Nyembo Christian, katibu wa kitaifa na mhamasishaji wa chama hicho, na Parole Kamizelo, afisa wa mawasiliano wa PPRD.

Hatimaye, Seth Kikuni, mwanachama wa vuguvugu la “Okoa DRC”, lililoanzishwa katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, karibu na Joseph Kabila, amechagua kukimbilia uhamishoni. Chama chake kinadai kwamba aliondoka DRC kwa kuhofia usalama wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *