Mlipuko wa Mpox barani Afrika haluko tena “dharura ya kiafya barani humo,” aetangaza Jean Kaseya siku ya Alhamisi, Januari 22. Mkurugenzi Mkuu wa Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) amesifu ubora wa mwitikio ulioratibiwa kwa ugonjwa huo, ambao unaweza kutumika kama mfano wa siku zijazo.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Hali ya dharura ilitangazwa mnamo mwezi Agosti 2024. Kufikia mwisho wa mwaka huo, zaidi ya watu 80,000 waliambukizwa virusi vya Mpox na watu 1,340 kufariki, huku Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ikihusika karibu visa vyote.

Mwaka mmoja na nusu baadaye, hali hii ya dharura imeondolewa.

Katika kipindi hicho, zaidi ya dola bilioni moja zilitengwa, mifumo ya ufuatiliaji na uchunguzi iliboreshwa sana, na dozi milioni 5 za chanjo zilisambazwa katika nchi 16. Kufikia mwisho wa mwaka 2025, idadi ya visa vilivyothibitishwa ilipungua kwa 60%, na kiwango cha vifo kutokana na ugonjwa huo kilipungua kutoka 2.6% hadi 0.6%.

Mafanikio haya yanakaribishwa na CDC Afrika, ambayo iliratibu juhudi hii. Hata hivyo, Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) vinasisitiza kwamba tangazo hili halimaanishi kwamba virusi havisambai tena: vinabaki kuwa vya kawaida katika maeneo kadhaa. Hata hivyo, zana sasa zipo ili kuhama kutoka kwa mwitikio wa dharura hadi awamu endelevu ya kuzuia na kudhibiti, inayoongozwa na nchi zenyewe.

CDC inaongeza kuwa mfumo huu wa usimamizi sasa utatumika kama mfano wa magonjwa mengine yenye uwezekano wa mlipuko, kama vile Kipindupindu, Dondakoo, Surua, na Polio.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *