
Baada ya Jukwaa la Davos, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Félix Tshisekedi yuko leo Ijumaa, Januari 23 Paris kwa mkutano na Emmanuel Macron kulingana na RFI.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Majadiliano yanatarajiwa kujikita kwenye masuala ya pande mbili pamoja na hali katika eneo la Maziwa Makuu, katika muktadha wa kikanda uliojaa mvutano unaoendelea.
Baada ya Jukwaa la Davos Jumatano, Januari 21, na kutua kwa muda mfupi huko Brussels, Félix Tshisekedi anakula chakula cha mchana leo mjini Paris na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron. Kulingana na vyanzo vyetu, mkutano huu unafanyika kwa ombi la Kinshasa. DRC ni nchi ya Afrika ambayo Ufaransa ilifanya nayo ahadi muhimu zaidi mwaka jana.
Maazimio mawili yaliyofadhiliwa na Paris
Kwa mfano, Ufaransa ilifadhili maazimio mawili ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu hali nchini DRC. Paris ilifanya hivo kama “mhusika,” ikimaanisha ilichukua jukumu la kuandika nakala, kufanya mazungumzo na wanachama wengine wa Baraza, na kuyawasilisha kwa kura.
Maazimio haya mawili yalikuwa magumu sana kujadili: la kwanza kutokana na kusita kwa nchi zingine za Afrika na majukumu ambayo yanaibua, na la pili kwa sababu linahusu agizo la MONUSCO, katika muktadha wa ushindani wa kijiografia kati ya Marekani na China katika eneo la Maziwa Makuu.
Jumla ya euro milioni 850 tayari zimetolewa
Majadiliano kati ya Félix Tshisekedi na Emmanuel Macron pia yanatarajiwa kuangazia Mkutano wa Paris wa Oktoba 30, 2025, kwa ajili ya amani na ustawi katika eneo la Maziwa Makuu. Kati ya euro bilioni 1.5 zilizoahidiwa katika tukio hili na mataifa 70 na mashirika ya kimataifa, ufadhili wote wa dharura wa kibinadamu, unaofikia euro milioni 850, tayari umetolewa, kulingana na Paris.
Wito wa mazungumzo kati ya Wakongo pia utajadiliwa. Msimamo wa Paris unajulikana sana: kufikia amani ya kudumu, na sambamba na mashauriano yanayofanywa na makanisa ya Kongo, Ufaransa inatoa wito wa kufanyika kwa mazungumzo ya kitaifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.