Kremlin imetangaza Ijumaa, Januari 23, mkutano wa pande tatu na Ukraine na Marekani katika Falme za Kiarabu baadaye siku hiyo, kufuatia mkutano ulioonekana kuwa “muhimu” kati ya Vladimir Putin na mjumbe wa Marekani Steve Witkoff huko Moscow.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Imeafikiwa kwamba mkutano wa kwanza wa kikundi kazi cha pande tatu kuhusu masuala ya usalama utafanyika leo huko Abu Dhabi,” mshauri wa Kremlin katika masuala ya diplomasia, Yuri Ushakov, amewaambia waandishi wa habari, akisisitiza kwamba mkutano kati ya Putin na Witkoff siku ya Alhamisi ulikuwa “muhimu kwa kila njia.” 

Kulingana naye, ujumbe wa Urusi, ukiongozwa na Jenerali Igor Kostyukov, afisa mkuu katika makao makuu ya jeshi, “utasafiri hadi Abu Dhabi katika saa zijazo.”

Habari zaidi zinakujia…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *