
Umoja wa Afrika (AU) umetangaza siku ya Alhamisi, Januari 22, kuondolewa kwa vikwazo dhidi ya Guinea, nchi ya Afrika Magharibi ambayo ilikuwa imesimamiswa taasisi za shirika hilo kufuatia mapinduzi ya mwezi Septemba 2021.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Baraza la Amani na Usalama la AU, ambalo limekaribisha kufanyika kwa uchaguzi wa urais uliofanya kuchaguliwa kwa Jenerali Mamadi Doumbouya mwishoni mwa mwezi Desemba, “limeamua kuondoa hatua ya kusimamishwa kwa ushiriki wa Jamhuri ya Guinea katika shughuli za AU,” kulingana na taarifa.
Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika limesema Guinea imepiga hatua katika utekelezaji wa mkakati wa kipindi cha mpito ambacho kiliishia kwa kuandaliwa kwa uchaguzi wa mwezi uliopita.
Umoja wa Afrika umempongeza kiongozi wa zamani wa jeshi Mamadi Doumbouya kwa kuchaguliwa kwake. Doumbouya aliapishwa kama rais Jumamosi iliyopita mbele ya maelfu ya wafuasi wake na marais kadhaa.
Doumbouya alimpindua rais Alpha Conde mwaka 2021 na tangu aingie madarakani alibinya uhuru wa kiraia na kupiga marufuku maandamano.