Kufuatia taarifa za watu wanaotumia namba za simu 0615 252 722 na 0766 116 687 na kujitambulisha kama waziri wa fedha na kuomba msaada wa kifedha kwa madai ya kuuguliwa au kuwa na msiba, Serikali imewatahadharisha wananchi na kusema kuwa watu hao wana lengo la kujipatia fedha kwa udanganyifu.
“Mtu yeyote atakayepokea simu au ujumbe wa aina hiyo anatakiwa kupuuza mara moja, kwani namba hizo si za Waziri wa Fedha,” – imesema taarifa ya Wizara ya Fedha iliyotolewa kwa umma .
Wizara hiyo imeeleza kuwa inafuatilia kwa karibu suala hilo kupitia vyombo vya dola ili kuwabaini na kuwachukulia hatua kali za kisheria wote wanaohusika na vitendo hivyo vya udanganyifu.
Aidha, wananchi wametakiwa kuwa makini na kuthibitisha taarifa zozote zinazohusisha viongozi wa serikali kabla ya kuchukua hatua yoyote, ili kuepuka kudanganywa na watu wasio waaminifu.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

(Feed generated with FetchRSS)