Mtaalamu wa Falsafa, Saikolojia na Stadi za Maisha, Siegfried Mbuya amesema misemo ya wahenga bado ina mchango mkubwa katika jamii ya sasa, akieleza kuwa misemo hiyo ina mafunzo muhimu yenye busara na hekima ambayo vijana wanaweza kujifunza na kuyatumia katika maisha ya kila siku.

Ameeleza zaidi kuwa ili kukabiliana na mabadiliko yanayoendelea katika jamii, kunahitajika ushirikiano kati ya vijana na wazee kwa kukaa pamoja na kubadilishana mawazo. Hatua hiyo, amesema, itasaidia kila upande kuelewa mitazamo ya mwenzake na kuoanisha maadili ya jadi na hali halisi ya maisha ya sasa.

#AzamTVUpdates
✍Halima Abdallah
Mhariri | John Mbalamwezi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *