TUNISIA; MAUMIVU kwa mashabiki wa Simba kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika yanaendelea msimu huu wa mwaka 2025/25, baada ya leo timu hiyo kufungwa bao 1-0 na Espérance de Tunis ya Tunisia mchezo uliofanyika nchini Tunisi.

Kutokana na matokeo hayo Simba imemaliza duru la kwanza la michuano hiyo ikiwa imepoteza michezo yote mitatu iliyocheza na inashika nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa kundi lake.

Kwenye michezo yake miwili iliyopita, Simba ilifungwa bao 1-0 na Petro de Luanda, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam kabla ya kufungwa mabao 2-1 na Stade Malien ugenini. Esperance ilitoka sare na Petro de Luanda ya Angola na Stade Malien ya Mali. Simba itarudiana na Esperance wiki ijayo Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

#MazingiraNiUtu
#27YaKijani #MitiniUhai #TanzaniaYaKijani
#HabarileoUPDATES

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *