Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwa ajili ya kumwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya marehemu Mzee Edwin Mtei, yanayofanyika Tengeru leo Jumamosi Januari 24, 2026 jijini Arusha.
Viongozi mbalimbali wa Serikali, familia, marafiki na wananchi wanatarajiwa kushiriki katika ibada na shughuli za mazishi ya kiongozi huyo wa zamani wa sekta ya fedha nchini.
Mzee Mtei aliyewahi kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuanzia mwaka 1966 hadi 1974, alifariki dunia usiku wa Januari 19, 2026 jijini Arusha.

(Feed generated with FetchRSS)