Afisa Mkuza Mitaala wa VETA, Thanasia Kisyeri, amesema kuwa sekta ya ubunifu wa mavazi ni miongoni mwa sekta zinazokua kwa kasi kubwa nchini akieleza kwa sasa VETA ina vyuo 59 kati ya vyuo 80 vinavyotoa elimu ya ubunifu wa mavazi, ambapo idadi kubwa ya wanafunzi wanajiunga na vyuo hivyo kutokana na uhitaji wa soko la ajira ndani na nje ya nchi.
Ameeleza kuwa, kwa mujibu wa mwelekeo wa soko la dunia na Tanzania kwa ujumla, sekta ya ubunifu wa mavazi inatoa fursa nyingi za kujiajiri pamoja na kuajiri wengine, hivyo kuwa kichocheo muhimu cha maendeleo ya vijana na uchumi wa Taifa.
✍ Roland John
Mhariri | @rajjmsangi
#AzamTVUpdates
(Feed generated with FetchRSS)