#HABARI: Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Yusuph Mwenda amesisitiza kuwa mpango kazi wa mamlaka hiyo ni kuhakikisha inaongeza ufanisi juu ya namna bora za kuwawezesha Mawakala wa Forodha kutimiza jukumu lao la msingi katika kulinda usalama wa Watanzania kupitia shughuli mbalimbali za forodha kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
Amebainisha hayo katika bonanza la michezo kwa ajili ya ufunguzi wa Siku ya Forodha Duniani ambayo kilele chake ni kesho yenye kauli mbiu Firodha Kufanya Kazi kwa Umakini Katika Kulinda Jamii kwa Umakini na Kujitoa.
Kwa upande wake Kamishna wa Idara ya Forodha na Ushuru wa Bidhaa wa Mamlaka hiyo amesema maadhimisho hayo yanakuja kama ukumbusho wa umuhimu wao kutekekeza majukumu yao katika udhibiti wa vitu visivyohitajika kuingia nchini.
Katika michezo iliyochezwa katika bonanza hilo TRA iliibuka kidedea kwa bao mbili kwa bila dhidi ya Mawakala wa Forodha huku michezo mingine ikiwa ni kuvuta kamba, kukimbiza kuku, kukimbia na magunia na mazoezi ya wote.
(Feed generated with FetchRSS)