
Katika Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) huko Davos, Uswisi, lililofanyika kuanzia Januari 19 hadi 23, 2026, Afrika Kusini ilitangaza “kujiondoa kwa muda” kutoka G20, huku Marekani ikishikilia urais wa mzunguko kwa mwaka 2026. “Afrika Kusini inataka kuepuka matatizo yoyote, mgogoro wowote na Marekani, na ni uamuzi wa busara kweli,” Koffi Kouakou, mhadhiri katika Shule ya Utawala katika Chuo Kikuu cha Witwatersrand huko Johannesburg, ameiambia RFI.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Hali hii ya mvutano si mpya. Mwezi Novemba mwaka uliyopita, Rais wa Marekani Donald Trump alisusia mkutano wa kilele wa G20 uliofanyika Afrika Kusini, akiishutumu nchi hiyo kwa kufuata sera zinazopinga maslahi ya Marekani.
Miezi miwili iliyopita, Pretoria ilitangaza kusitishwa kwa mwaka mmoja kwa ushiriki wake katika mkutano wa kilele wa G20 wa 2026, kujiondoa ambako sasa kunachukua sura halisi kwa kujiondoa huku kwa muda kutoka kwa kundi la mataifa ishirini yenye uchumi mkubwa zaidi duniani.
Kwa hivyo, katika hatua adimu, karibu isiyo ya kawaida, G20, mnamo mwaka 2026, inakuwa, kwa njia fulani, G19 huku Afrika Kusini ikiondoka kwa muda kutoka kwa kundi hilo.
Hakika, Pretoria inalaani waziwazi hali ya kisiasa ambayo imekuwa ni tatizo chini ya urais wa Marekani.
“Uamuzi thabiti, wa busara, na wa hekima”
Akiwasiliana na RFI, Koffi Kouakou, mhadhiri katika Shule ya Utawala katika Chuo Kikuu cha Witwatersrand huko Johannesburg, anabainisha kwamba uamuzi huo ni wa kimantiki na unaeleweka: “Ni uamuzi thabiti, wa busara, na wa hekima.” G20, ambayo iliundwa ili kuunganisha nchi zote za dunia, si zile tunazopenda tu, zile zinazofanana nasi, au zile zilizo kama sisi, sasa inaangamizwa na Rais Trump. Ni aibu kweli. Lakini Afrika Kusini inataka kuepuka matatizo yoyote, mgogoro wowote na Marekani, na ni uamuzi wa kimantiki sana.
Pretoria inazungumzia rasmi kuondoka kwa muda, lakini kujiondoa hukutakuwa na athari, hasa kwa uwakilishi wa bara la Afrika.
“Kujiondoa kwake kutaifanya Afrika isiwezi kuwakilishwa…”
“Ni ishara kali sana, na wanachama wa G20 lazima wafikirie hilo kwa sababu pia kutakuwa na athari kwa jukumu la Umoja wa Afrika.” Afrika Kusini na Umoja wa Afrika zinawakilisha karibu watu bilioni 1.4. “Kujiondoa kwake kutaifanya Afrika isiwezi kuwakilishwa, Afrika haitaweza kuwakilishwa ndani ya G20,” ameongeza Koffi Kouakou.
Mwaka ujao, Uingereza itachukuwa urais wa kupokezana wa G20. Pretoria inatumai hali ya amani zaidi ya kidiplomasia na kurudi kwenye meza ya kundi la nchi zenye uchumi mkubwa duniani.