WAFANYABIASHARA wadogo wa nguo za mitumba katika soko maarufu la Orofea, lililopo Kata ya Mshindo katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, wamelalamikia uchakavu wa miundombinu ya soko hilo, hususan paa ambalo wamesema linavuja wakati wa mvua, hali inayosababisha bidhaa zao kuharibika na kuwafanya kufanya biashara katika mazingira magumu, hivyo kuathiri kipato na ustawi wao kwa ujumla.

Wametoa kilio hicho wakati wa ziara ya kazi ya Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Fadhili Ngajilo kwenye soko hilo.

Wamesema soko hilo ni chakavu hali ambayo inafanya sehemu kubwa ya miundombinu sokoni hapo kuwa si rafiki na hivyo kufanya ufanyaji biashara kuwa mgumu wakati wote wa jua au mvua.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *