#HABARI: Awamu ya kwanza ya mradi wa Mabasi yanayotumia Umeme (Zan Bus), imewasili kupitia Bandari ya Malindi, Zanzibar, na kuelekea katika maegesho ya Stendi Mpya ya Kijangwani, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Mabasi hayo yanatarajiwa kuanza kutoa huduma rasmi za usafiri wa abiria mwezi Februari, hatua inayolenga kupunguza msongamano wa magari barabarani pamoja na kuboresha usafiri rafiki wa mazingira Zanzibar.

Mradi huo unatarajiwa kuendelea kutekelezwa hatua kwa hatua, unaratibiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) na utasimamiwa na Kampuni ya Usafirishaji ya Unitrans kutoka Afrika Kusini.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *