#HABARI: Moto mkubwa umezuka usiku wa kuamkia leo Januari 26, 2026 katika eneo la Moshono, jijini Arusha, na kuteketeza maduka kadhaa pamoja na karakana ya mbao, tukio lililosababisha hasara kubwa ya mali.
Kwa mujibu wa taarifa za awali kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo, moto huo ulianza majira ya saa tisa usiku na kuenea kwa kasi, hali iliyochangiwa na uwepo wa mbao nyingi na vifaa vinavyoshika moto kwa urahisi.
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji liliwasili katika eneo la tukio na kuanza mara moja juhudi za kuuzima moto huo, kwa lengo la kuzuia usienee katika makazi ya jirani
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.