Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, Mbarouk Salim Mbarouk, amefunga mafunzo ya siku tatu kwa wasimamizi wa uchaguzi Mjini Iringa na kuwataka watendaji hao wa tume kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi, weledi na kwa kuzingatia kikamilifu sheria, kanuni na miongozo ya nchi ili kufanikisha zoezi la uchaguzi mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Peramiho mkoani Ruvuma na Udiwani katika Kata ya Shiwinga mkoani Songwe.
Uchaguzi huo mdogo kwenye maeneo hayo nchini unatarajiwa kufanyika Tarehe 26 Februari 2026.
(Feed generated with FetchRSS)