Wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa wameonya siku ya Jumapili kwamba kuongezeka kwa vurugu nchini Sudan Kusini kunaongeza hatari ya ukatili mkubwa dhidi ya raia, wakitaja mapigano mapya na maneno ya uchochezi. Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema ina wasiwasi mkubwa na mapigano katika jimbo la Jonglei, ambapo mashahidi wameripoti raia kukimbilia kwenye vinamasi vilivyo karibu.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Hali nchini Sudan Kusini inaongeza hatari ya vurugu kubwa dhidi ya raia, wataalam huru wa Umoja wa Mataifa walionya Jumapili, huku migogoro mipya na maneno ya vurugu yakiikumba nchi hiyo.

Katika taarifa, Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini ilionyesha “wasiwasi wake mkubwa” kuhusu mapigano katika Jimbo la Jonglei, kaskazini mwa mji mkuu Juba, ambapo mashahidi walielezea raia wakikimbia kwenye vinamasi.

Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Sudan Kusini (SSPDF), Lul Ruai Koang, aliwaambia wakazi wa Jonglei siku ya Jumapili jioni kwamba lazima “waondoke mara moja” maeneo yanayodhibitiwa na waasi wa SPLA-IO na kutafuta hifadhi “haraka iwezekanavyo katika maeneo yanayodhibitiwa na serikali.”

“Raia watachukuliwa kuwa lengo halali za kijeshi,” msemaji huyo aliongeza.

Nchi hiyo changa zaidi duniani imekuwa ikikumbwa na vita, umaskini, na ufisadi ulioenea tangu kuanzishwa kwake mwaka wa 2011, na vurugu kati ya makundi hasimu zinaongezeka tena.

Makubaliano ya kugawana madaraka kati ya kambi hizo mbili kuu yamezima na wala hakuna matumaini ya kuyafufua tangu Rais Salva Kiir alipochukua hatua dhidi ya makamu wake wa rais na mpinzani wake wa muda mrefu, Riek Machar, ambaye alikamatwa mwezi Machi mwaka uliyopita na kwa sasa anasughulikiwa na mahakamakwa uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Vikosi vyao vimepambana mara kadhaa mwaka uliopita, lakini mapigano makali zaidi yalianza mwishoni mwa mwezi Desemba katika Jimbo la Jonglei.

Matamko ya umma ya makamanda wanaochochea vurugu dhidi ya raia, pamoja na uhamasishaji wa wanajeshi, “yanafanya ongezeko hatari wakati ambapo misingi ya kisiasa ya mchakato wa amani tayari imedhoofika,” tume ya Umoja wa Mataifa imesema.

Mkuu wa Jeshi Paul Nang Majok aliamuru wanajeshi waliotumwa katika eneo hilo siku ya Jumatano “kuangamiza uasi” ndani ya siku saba.

Vyombo vya habari vya ndani pia vimeripoti kwamba afisa mkuu wa jeshi alisema, “Hakuna anayepaswa kuachwa, hata wazee.”

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS) ulisema “una wasiwasi mkubwa” na matamshi haya ya umma.

“Matamshi ya uchochezi yanayotaka vurugu dhidi ya raia, haswa walio hatarini zaidi, ni ya kuchukiza kabisa na lazima yasitishwe mara moja,” amesema Graham Maitland, mkuu wa UNMISS.

Mapigano mapya nchini Sudan Kusini yamesababisha watu zaidi ya 180,000 kuyatoroka makazi yao, kulingana na mamlaka ya nchi hiyo.

Kiir na Machar walipigana vita vya miaka mitano muda mfupi baada ya uhuru, ambavyo viligharimu maisha ya watu 400,000. Makubaliano ya kugawana madaraka yaliyofikiwa mwaka wa 2018 yalidumisha amani kwa miaka michache, lakini mipango ya uchaguzi na muunganiko wa vikosi vya jeshi haikufanikiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *