Rais wa Brazil Lula amemwomba mwenzake wa Marekani Donald Trump siku ya Jumatatu, Januari 26, kuliwekea kikomo “Baraza lake la Amani” kuhusu suala la Gaza, wakati wa mazungumzo ya simu ambapo wamekubaliana kukutana Washington, kulingana na Brasilia.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Luiz Inacio Lula da Silva, aliyealikwa kama wengine kushiriki katika “Baraza la Amani” lililofikiriwa na Donald Trump, alipendekeza kwamba shirika hili “liwekewe kikomo kwenye suala la Gaza na lijumuishe kiti cha Palestina,” wakati wa mazungumzo ya dakika 50, kulingana na taarifa kutoka kwa ofisi ya rais wa Brazil.

Kiongozi huyo wa Brazil “alisisitiza umuhimu wa mageuzi kamili ya Umoja wa Mataifa, ikiwa ni pamoja na kupanua wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama.”

Siku ya Ijumaa, alimtuhumu Rais wa Marekani Donald Trump kwa kutaka kuwa “msimamizi” wa “Umoja wa Mataifa mpya” kwa kuundwa kwa “Baraza la Amani.”

Hapo awali, ikiwa ni sehemu muhimu ya mpango wa kukomesha vita katika eneo la Palestina la Ukanda wa Gaza, shirika hili linaonekana kuwa na matarajio mapana zaidi, na kuifanya kuwa mbadala wa Umoja wa Mataifa.

Lula na Donald Trump wamekuwa wakiwasiliana mara kadhaa tangu mkutano wao wa kwanza rasmi mnamo mwezi Oktoba, baada ya miezi kadhaa ya mgogoro kati ya Washington na Brasilia. Kufuatia kuanzishwa kwa mahusiano haya, utawala wa Marekani ulifuta hatu yakedhidi ya bidhaa nyingi za Brazil ambazo zililengwa na ushuru wa 40% uliowekwa na Marekani. Pia iliondoa vikwazo dhidi ya jaji wa Brazil.

Lula na Trump wajadili Venezuela

Kulingana na taarifa kutoka Brasilia, marais wa Marekani na Brazil pia walijadili hali nchini Venezuela: Lula alitoa wito wa “kuhifadhi amani na utulivu katika eneo hilo.”

Kufuatia kutekwa nyara kwa rais wa Venezuela Nicolas Maduro wakati wa operesheni kubwa ya kijeshi ya Marekani mapema mwezi Januari, Lula alilaani kitendo ambacho “kinavuka mstari wa kile kinachokubalika.”

Wakati wa mkutano wao, marais wa Brazil na Marekani “walikubaliana” kuhusu ziara ya rais Luiz Inacio Lula da Silva huko Washington.

Itafanyika baada ya ziara za mkuu wa nchi wa Brazil kwenda India na Korea Kusini mwezi Februari, na tarehe itatangazwa “hivi karibuni,” ofisi ya rais wa Brazil imesema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *