Serikali imesema imeshaanza mazungumzo na Qatar kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano kwa ajili ya kusaini makubaliano ya kuongeza fursa za ajira kwa vijana wa Kitanzania.

Akizungumza kando ya Mkutano wa Mawaziri wa Kazi Duniani (Global Labour Market Conference) unaofanyika Jijini Riyadh, Saudi Arabia na kushirikisha mawaziri wa kazi kutoka nchi 45, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu amesema forsa za kazi na ajira ambazo Tanzania zinaendelea kuzitafuta zinahusiana na sekta mbalimbali zikiwemo sekta za ujuzi.

Msikilize.

Mhariri @moseskwindi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *