Rais wa Marekani Donald Trump wa Marekani amesema utawala wake unafikiria kupunguza operesheni za wahamiaji wasio na vibali kwenye mji wa Minneapolis baada ya maafisa wa kikosi maalum cha uhamiaji ICE) kuwaua watu wawili.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Washington inakumbwa na msukosuko wa kisiasa siku tatu baada ya kifo cha Alex Pretti huko Minneapolis, aliyeuawa na maafisa wa polisi wa mpakani (ICE). Warepublican wanadai uwajibikaji, huku Wademokrat wakitishia kuzuia bajeti za mashirika ya vikosi vya usalaama, baada ya vifo vya watu wawili katika operesheni za maalum cha uhamiaji (ICE)

Siku tatu baada ya maafisa uhamiaji kumpiga risasi na kumuua raia mwingine wakati wa operesheni ya polisi dhidi ya wale inaowashuku kutokuwa na vibali, rais wa Marekani alisema utawala wake utapunguza operesheni yake ya kuwasaka wahamiaji haramu mjini Minneapolis.

Kufuatia mkasa huo, Trump tayari alitangaza kuondolewa kwa aliyekuwa kiongozi wa oparesheni ya kuwasaka wahamiaji kwenye mji wa Minneapolis na hapo jana alimtuma mkuu wa ulinzi wa mipaka ya nchi hiyo kwenda kwenye mji huo kutuliza hasira ya umma.

Mauaji haya yalichochea wimbi la maandamano ya umma na shutuma kali. Wakati huo huo Waziri wa Usalama wa Nchi, Kristi Noem, anakabiliwa na shinikizo la kujiuzulu.

Viongozi wa Democratic bungeni wametishia kupiga kura ya kutokuwa na imani naye iwapo Rais Trump hatamfuta kazi. 

Kambi ya Republican ina wasiwasi na inahitaji maelezo. Angalau maseneta wa Republican wanatoa wito wa uchunguzi wa kina na wakuu wa ICE na polisi ya ulinzi wa mpaka waitwe. Hali hii inaonesha ghasia zaidi kuliko kawaida ndani ya chama cha Donald Trump. Kwa mfano, hakukuwa na jibu lolote wakati wa kutekwa nyara kwa rais wa Venezuela Nicolas Maduro, ni maoni machache tu yaliyosikika kuhusu Greenland.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *