
Wakati wa mazungumzo ya simu na Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman, Rais wa Iran Massoud Pezeshkian amesisitiza kwamba ukosefu wa utulivu wa kikanda “haufaidii mtu yeyote.”
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Rais wa Iran Massoud Pezeshkian alizungumza kwa simu na Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman (MBS) baada ya kuwasili kwa meli kubwa ya kivita ya Marekani katika eneo hilo, huku kukiwa na hofu ya kuongezeka kwa mgogoro mpya na Israel au Marekani.
Katika wiki za hivi karibuni, Marekani imeonyesha kuwa inafikiria kushambulia Iran kujibu ukandamizaji wa Tehran dhidi ya waandamanaji, ambao umewaua maelfu ya watu. Rais wa Marekani Donald Trump alituma meli kubwa ya kibita USS Abraham Lincoln katika eneo hilo.
Bw. Pezeshkian alilaani “vitisho” vya Marekani wakati wa mazungumzo yake ya simu na kiongozi wa Saudi Arabia siku ya Jumanne, akisema kwamba “vitisho hivyo vinalenga kuvuruga usalama wa kikanda na haivtachangia chochote ispokuwa kuhatarisha usalama.”
“Rais alizungumzia shinikizo na uhasama wa hivi karibuni dhidi ya Iran, ikiwa ni pamoja na shinikizo za kiuchumi na uingiliaji kati wa kigeni, akisema kwamba vitendo hivi havikufanikiwa kudhoofisha uthabiti na umakini wa raia wa Iran,” ofisi ya Pezeshkian ilisema katika taarifa Jumanne.
Taarifa hiyo pia ilibainisha kuwa Mwanamfalme Mohammed “alikaribisha mazungumzo hayo na kuthibitisha tena kujitolea kwa Saudi Arabia kwa utulivu, usalama, na maendeleo ya kikanda.”
“Alisisitiza umuhimu wa mshikamano miongoni mwa nchi za Kiislamu na akasema kwamba Riyadh inakataa aina yoyote ya uchokozi au kuongezeka kwa vurugu dhidi ya Iran,” taarifa hiyo imeongeza, ikibainisha kwamba alielezea nia ya Riyadh ya kuanzisha “amani na usalama katika eneo lote.”
Shirika la Habari la serikali ya Saudi Arabia (SPA) liliripoti baada ya mazungumzo kwamba Mwanamfalme Mohammed alimwambia Pezeshkian kwamba Riyadh haitaruhusu matumizi ya anga yake au eneo lake kwa vitendo vya kijeshi dhidi ya Tehran.
“Wakati wa mazungumzo ya simu, Mwanamfale amebaiinisha msimamo wa nchi yake kuhusu heshima kwa uhuru wa Iran, akisisitiza kwamba Saudi Arabia haitaruhusu matumizi yoyote ya anga au eneo lake kwa vitendo vya kijeshi dhidi ya Iran au kwa mashambulizi, kutoka kwa asili yoyote au upande wowote” SPA Shirika la Habari la serikali ya Saudi Arabia (SPA) limeripoti.