Mfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman ameapa akisisitiza kwamba ardi ya ardhi ya nchi yake haitotumika kuishambulia Iran. Hayo alimuahikishia Rais wa Iran Masoud Pezeshkian siku ya Jumanne, wakati wa mazungumzo ya simu kati ya viongozi hao wawili.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mwanamfalme wa Saudi Arabia “amebainisha wakati wa mazungymzo ya simu msimamo wa Saudi Arabia kuhusu kuheshimu uhuru wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kubainisha kwamba nchi yake haitaruhusu anga yake au eneo lake kutumika kwa vitendo vya kijeshi dhidi ya Iran,” Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi Arabia imesema katika taarifa.

Kauli hii ya Mwanamfale Bin Salman inakuja wakati kuna wasiwasi kwamba Marekani inaweza kuishambulia Iran baada ya kuituhumu serikali ya nchi hiyo kufanya mauaji na ukandamizaji kwa maandamano ya amani ya kiraia yaliyofanyika mapema mwezi huu.

 Rais wa Marekani Donald Trump alituma meli kubwa ya kibita USS Abraham Lincoln katika eneo hilo.

Bw. Pezeshkian alilaani “vitisho” vya Marekani wakati wa mazungumzo yake ya simu na kiongozi wa Saudi Arabia siku ya Jumanne, akisema kwamba “vitisho hivyo vinalenga kuvuruga usalama wa kikanda na haivtachangia chochote ispokuwa kuhatarisha usalama.”

“Rais alizungumzia shinikizo na uhasama wa hivi karibuni dhidi ya Iran, ikiwa ni pamoja na shinikizo za kiuchumi na uingiliaji kati wa kigeni, akisema kwamba vitendo hivi havikufanikiwa kudhoofisha uthabiti na umakini wa raia wa Iran,” ofisi ya Pezeshkian ilisema katika taarifa Jumanne.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *