Serikali imeendelea kuboresha huduma za watoto wachanga wanaozaliwa kabla ya wakati (watoto njiti) katika vituo vya afya nchini, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuboresha afya ya mama na mtoto.
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Florence Samizi amesema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Christina Solomon Mndeme leo Januari 28, 2026 bungeni jini Dodoma, aliyetaka kujua Je, Serikali ina mkakati gani wa kupanua wigo wa huduma za Watoto Njiti katika vituo vya afya vya mkoa wa Tabora.
Amesema Serikali imefanikiwa kuongeza vituo vinavyotoa huduma za watoto njiti kutoka hospitali 14 pekee mwaka 2018 hadi kufikia hospitali 362 mwaka 2025 kote nchini. Dkt. Samizi ameongeza kuwa kwa mkoa wa Tabora, huduma hizo zimepanuliwa kutoka vituo sifuri mwaka 2018 hadi kufikia vituo 33 mwaka 2025, hali inayochangia kwa kiasi kikubwa kuimarika kwa huduma za watoto wachanga wanaozaliwa kabla ya wakati pamoja na watoto wachanga wagonjwa.
#StarTvUpdate
(Feed generated with FetchRSS)