Taasisi ya Mama Asemewe imesema Tanzania nzima imepanda Miti Jana Januari 27, 2026 kumuunga Mkono Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyekuwa akisherehekea kumbukizi ya kuzaliwa kwake, kama ishara ya Rais Samia kutambua na kuenzi uhai wa mwanadamu.

Akizungumza kwaniaba ya Taasisi hiyo, Mwenyekiti wake Bw. Geofrey Kiliba akiwa Dar Es Salaam kwenye Kusanyiko kubwa la Vijana wa Taasisi hiyo, amesema kupanda miti kulikoongozwa na Rais Samia ni ishara ya upandaji wa wema wake katika kuchagiza ongezeko la rasilimali maji kutokana na namna ambavyo miti imekuwa na mchango wa upatikanaji wa maji na hewa safi kote nchini.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *