Tehran imeionya Washington dhidi ya uvamizi wa aina yoyote kwenye ardhi yake. Onyo hilo limetolewa jana na mshauri mkuu wa kiongozi wa juu wa Iran, Ali Shamkhani, ambaye amesema kuwa shambulio lolote la kijeshi la Marekani dhidi ya Iran litachukuliwa kama tangazo la vita.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Iran imesema itajibu mapigo hadi Tel Aviv iwapo Marekani itathubutu kuishamb Jeshi la Iran na walinzi wa mapinduzi pia wamesema wako tayari kwa hali zote za kivita. Onyo hilo lililotolewa jana Jumatano linajibu kitisho cha Rais Donald Trump cha kuiingilia kijeshi nchini Iran.

Msemaji wa walinzi wa mapinduzi, Ali Mohammad Naeini, alionya kuwa uzoefu wa vita vya awali umeonyesha kushindwa kijeshi dhidi ya Iran, akisisitiza kuwa majeshi ya Iran ndiyo yataamua mwisho wa mapambano.

Wakati huo huo Iran imetangaza kuwa imejumuisha mji wa Tel Aviv katika orodha ya maeneo itakayoshambulia iwapo itashambuliwa na Marekani au washirika wake, ikionya kuwa itajibu kwa haraka, kwa shambulilo lisilo na kifani.

Naye rais Donald Trump ameionya Iran kwamba “muda unakwisha” wa kujadili makubaliano kuhusu mpango wake wa nyuklia kufuatia ongezeko la vikosi vya kijeshi vya Marekani katika eneo la Ghuba.

Marekani imekuwa ikiishtumu Iran kwa kukandamiza kwa nguvu maandamano ya amani ya raia bila sababu zozote.

Hata hivyo, Iran imekanusha madai ya udhaifu wa ndani, ikieleza kuwa maandamano ya hivi karibuni ni njama za kigeni. Serikali ya Tehran imesisitiza kuwa itatetea mamlaka, uhuru na mfumo wake kwa nguvu zote endapo itakabiliwa na shambulio lolote la kijeshi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *