
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Niamey umekumbwa na ssintofahamu siku ya Jumatano usiku. Milipuko mikubwa na milio mikubwa ya risasi imeripotiwa usiku katika eneo hilo. Utulivu umerejea, lakini utambulisho wa washambuliaji haujulikani na hakuna takwimu za majeruhi zinazopatikana kwa wakati huu.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Majibizano ya risasi yalianza muda mfupi baada ya saa sita usiku katika eneo la Uwanja wa Ndege wa Diori Hamani kusini mashariki mwa Niamey. Hapa ndipo Kituo cha Jeshi la Anga la Niger 101 na kambi ya ndege zisizo na rubani zinapatikana. Shehena kubwa ya uranium pia imehifadhiwa katika eneo hili ikisubiri kusafirishwa nje.
Makao makuu ya Kikosi cha Kupambana na wanajihadi, kilichoundwa na Niger, Burkina Faso, na Mali, pia yapo eneo hilo.
Chanzo cha majibizano ya risasi jana usiku hakijulikani, kama vile utambulisho wa washambuliaji, lakini picha zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha mistari angavu angani, ikionyesha kwamba ulinzi wa anga huenda ulianzishwa, labda kutokana na shambulio la ndege zisizo na rubani.
Kwa vyovyote vile, milio ya risasi ilisababisha hofu miongoni mwa abiria kwenye uwanja wa ndege. Baadhi walikimbia eneo la tukio kwa miguu. Ndege zililazimika kuelekezwa kwenye viwanja vingine vya ndege.
Utulivu ulirejeshwa ndani ya saa moja, lakini hakuna takwimu za majeruhi zilizopatikana kufikia leo Alhamisi asubuhi.