Trump aliandika katika ukurasa wake wa kijamii kwamba anatumai Iran itakuja haraka katika meza ya mazungumzo na kuwa na makubaliano na kuelewa kuwa haipaswi kuwa na silaha za nyuklia. 

Kutokana na uwepo wa Vikosi vya Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati, rais Trump aliyeiondoa Marekani katika makubaliano ya Nyuklia ya Iran yaliyofikiwa mwaka 2015 wakati wa muhula wake wa kwanza, alisema onyo lake la mwisho kwa Iran, lilifuatiwa na shambulizi kubwa la kijeshi mwezi Juni na kusababisha mauaji ya makamanda wa kikosi maalum cha walinzi mapinduzi huku akionya kuwa shambulizi jengine dhidi ya nchi hiyo litakuwa kali zaidi.

Trump ameonya kuwa meli za kijeshi za Marekani tayari ziko njiani kuelekea Iran. Hata hivyo Iran imejibu vikali na kusema hatua zozote dhidi ya nchi yake pia zitakuwa na majibu makali. Ali Shamkhani, mshauri wa kiongozi wa juu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei, amesema shambulizi lao litalenga kambi za kijeshi za Marekani, Israel na mataifa mengine yoyote yanayowaunga mkono.

Iran itajibu shambulizi lolote kutoka Washington

Naye Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Iran Abbas Araqchi, amesema vikosi vyao maalum viko tayari kupambana na uchokozi wa ina yoyote. Lakini wakati huo huo Araqchi aliongeza kuwa nchi yake iko tayari kwa makubaliano yasiokuwa na upendeleo, yaliyo na faida kwa pande zote, yaliyo huru na yasiokuwa na vitisho.

Russland Moskau 2025 | Abbas Araqchi
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Iran Abbas AraqchiPicha: Alexander Miridonov/Kommersant Photo/Sipa USA/picture alliance

Amesema makubaliano hayo yanapaswa kuhakikisha Iran ina haki ya kuwa na teknolojia ya nyuklia akisema lakini nchi hiyo haina nia ya kumiliki silaha za nyuklia.

Wakati huo huo Umoja wa Ulaya umejipanga kuiwekea kuwawekea vikwazo vikosi maalum vya walinzi mapinduzi wa Iran, kufuatia kukamatwa waandamanaji wanaoipinga serikali. Hali hiyo inazidi kuipa wasiwasi Iran ambayo tayari inakabiliwa na kitisho hicho cha kushambuliwa kijeshi na Marekani iwapo waandamanaji zaidi wataendelea kuuwawa. Wanaharakati ndani na nje ya Iran wanadai zaidi ya

waandamanji 6000 wameuwawa katika wiki kadhaa za maandamano nchini humo huku wengine wengi wakikamatwa. Vikwazo vya EU kwa Iran pia huenda vikaudhoofisha zaidi uchumi wa taifa hilo ambao ni dhaifu kufuatia vikwazo vya kimataifa. Tayari sarafu ya taifa hilo imeshuka huku gharama ya maisha ikizidi kupanda.

Wairani walioko nje ya nchi wanawasiwasi na familia zao Tehran

Hadi sasa lakini haijawa wazi kuhusu nguvu atakayoitumia Trump dhidi ya taifa hilo, lakini baadhi ya wairan walioko nje ya nchi wanawasiwasi kuhusu jamaa zao kufuatia changamoto pia za mawasiliano, kama anavyosimulia Ario Kavousi:

Iran Teheran 2026 | Maandamano ya kupinga serikali
Maandamano ya kupinga serikali Iran, yamesababisha mauaji ya zaidi ya watu 6000 hii ikiwa ni kulingana na wanaharakati wa ndani na nje ya Iran. Picha: SalamPix/ABACA/IMAGO

“Inatisha sana, kila siku najaribu kuwapigia simu familia yangu, ili tu kuona kama wako sawa, ninajaribu njia zote ninazoweza, lakini inatisha sana. Naona jumbe hazifiki, ninapopiga simu nasikia tu ujumbe unaosema pole hatuwezi kuku kukuunganisha na nambari hii jaribu tena baadaye. Kinachoniogopesha kama nilivyosema hapo mwanzi ni kwamba sijui kama jaa zangu wapo hai au wamekufa.”

Tayari nchi za mashariki ya kati zinawasiwasi kufuatia shambulizi la Marekani dhidi ya Iran huku Uturuki ikipanga mikakati ya kuweka katika mipaka yake iwapo shambulizi hilo litatoklea.

Saudi Arabia na Umoja wa Falme za kiarabu wameashiria kuwa hawatokubali anga zao zitumike kwa shambulizi lolote lile. Lakini Marekani imeendelea na mipango yake ya kupeleka meli zake za kivita katika eneo hilo kwa nia ya kuishambulia Iran.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *