Wakulima nchini wanatarajiwa kunufaika na matumizi ya nishati ya jua katika shughuli za kilimo, hatua inayotarajiwa kupunguza gharama za uzalishaji, kuongeza tija mashambani na kuboresha uhifadhi wa mazao, hususan katika maeneo ya vijijini yenye changamoto ya upatikanaji wa umeme wa uhakika.

Kupitia teknolojia hiyo, wakulima wataweza kutumia umeme wa jua katika shughuli muhimu za kilimo ikiwemo umwagiliaji, uhifadhi wa mbegu na dawa katika majokofu, pamoja na uhifadhi wa mazao baada ya mavuno. Hatua hii inarahisisha utekelezaji wa kilimo cha kisasa na kupunguza utegemezi wa nishati ghali na zisizo rafiki kwa mazingira.

Hii inatokana na mkataba uliofikiwa hivi karibuni kati ya Chama cha Wakulima Tanganyika (TFA) na Kampuni ya Teknolojia ya Nishati ya Zola

Wakati wa hafla ya kusaini mkataba huo, Mkurugenzi Mtendaji wa TFA, Justin Shirima am,esema TFA itawasaidia wanachama wake kupata vifaa vya nishati ya jua kwa mfumo wa malipo madogo madogo, huku Zola ikitoa elimu ya teknolojia hiyo na kuhakikisha huduma za nishati safi zinapatikana kwa wakulima.

Mkataba huu unalenga kuwezesha wakulima wengi kumudu matumizi ya nishati ya jua na kuendeleza kilimo chenye tija.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Zola, Johnson Kiwanko amesema Kampuni hiyo ya kiteknolojia inayotumia akili mnemba (AI) katika utoaji wa huduma za Nishati, imeona uhitaji mkubwa wa nishati ya sola kwa wakulima nchini jambo lililoichochea kuingia mkataba huo.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *